Dodoma FM

Dodoma kuanza awamu yapili ya msaada wa kisheria

30 April 2026, 17:41

Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiongea na waandishi wa habari.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kituo kitakuwa Uwanja wa Mtekelezo, mkabala na Msikiti wa Gadaf ,Halmashauri ya Wilaya Chamwino vituo vitakuwa katika Ofisi ya Kijiji Buigiri, Kata ya Chinangali na Ofisi ya Kata Mlowa Barabarani ,Halmashauri ya Wilaya Kongwa vituo vitakuwa katika Ofisi ya Kata ya Kibaigwa na Ofisi ya Kata ya Mkoka.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameutangazia Umma kuhusu kuanza kwa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma kupitia Kampeni ya ‘Msaada wa Kisheria ya Mama Samia’ awamu ya Pili.

Aliongeza kuwa, katika utekelezaji uliofanyika 2023, Mkoa ulipata bahati ya kuwa wa kwanza kuanza utekelezaji wa Kampeni hiyo yenye manufaa makubwa kwa wananchi kwani jumla ya wananchi 86,947 wakijumuisha Wanaume 42,298 na Wanawake 44,649 walifikiwa na kupatiwa huduma za Msaada wa Kisheria.

Aidha, kati ya migogoro 818 iliyopokelewa, migogoro 452 ilitatuliwa na migogoro 366 inaendelea kufanyiwa kazi. Pamoja na mafanikio hayo, Serikali imeona bado kuna uhitaji na umuhimu wa kuendeleza juhudi za kuhakikisha wananchi wanapata huduma za msaada wa kisheria kwa urahisi na kwa wakati.

Kampeni hiyo itaanza rasmi Mkoa wa Dodoma Mei Mosi hadi 15, 2026 ambapo huduma zifuatazo zitatolewa bila malipo; ushauri wa kisheria, elimu ya masuala ya kisheria, uandaaji wa nyaraka za kisheria, uwakilishi Mahakamani na katika Mabaraza kwa wananchi wenye mashauri au wanaotaka kufungua mashauri, utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala na huduma ya usajili wa vyeti vya kuzaliwa na vifo kupitia RITA.

Elimu kwa jamii itatolewa katika ngazi ya Wilaya, Kata, Mitaa/Vijiji sambamba na kufanyika katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya wananchi kama vile masoko, vituo vya mabasi, mikusanyiko ya kijamii na taasisi za elimu. Aidha, kutakuwa na vituo vya huduma katika maeneo yafuatayo.

Sauti ya Mhe. Rosemary Senyamule,.