Dodoma FM

Wajawazito watakiwa kuzingatia mlo kamili

21 May 2026, 17:54

Ni vizuri akina mama wajawazito wakatumia vyakula vyenye protini, vitamin, madini, wanga pamoja na mbogamboga.Picha na mtandao.

Elimu inayotolewa kliniki ni muhimu Kwa maendeleo ya mama mjamzito na mtoto.

Na Victor Chigwada.

Akina mama wajawazito wametakiwa kula vyakula vyenye virutubisho ili waweze kujifungua salama na kupata watoto wenye afya bora.

Wito huo umetolewa na kaimu Afisa lishe wa mtaa wa Ihumwa A Bi. Maria Lyimo ambapo amesema kuwa akina mama wajawazito wengi hupata matatizo ya uzazi na kupelekea mimba kuharibika kutokana na kula vyakula visivyokuwa na virutubisho sahihi.

Amesema ni vizuri akina mama wajawazito wakatumia vyakula vyenye protini, vitamin, madini, wanga pamoja na mbogamboga kwa ajili ya kuwasaidia kukidhi ongezeko la mahitaji ya mwili wakati wa kipindi cha ujauzito.

Sauti ya Bi. Maria Lyimo.

Bi.Maria ameongeza kuwa ni vema mama mjamzito na mwenza wake kufika kliniki kupata mafunzo ya rishe Bora Kwa mama mjamzito pamoja na mtoto wa chini ya miaka miatano ili kuepuka utapiamlo Kwa watoto.

Sauti ya Bi. Maria Lyimo.

Nao baadhi ya akina mama wamesema elimu inayotolewa kliniki ni muhimu Kwa maendeleo ya mama mjamzito na mtoto wake kwani inampa fursa ya kupata elimu ya vyakula bora kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua.

Sauti za wanawake.