Fikra potofu, ukosefu wa ajira wazazi washawishi watoto wajifelishe
10 July 2026, 18:28

Hata hivyo baadhi Wazazi kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya faida za elimu, wamekuwa wakiwahimiza watoto wao kuolewa badala ya kuendelea na masomo.
Na Victor Chigwada.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ikombolinga wameendelea kushikilia dhana ya ukosefu wa ajira kwa kuwakosesha watoto haki ya kupata elimu wakiamini hata watoto hao wakisoma hakuna manufaa.
Mwenyekiti wa maendeleo katika Kata hiyo Bw.Mtemi Matonya amesema yapo maeneo yenye mwitikio mzuri wa elimu katika Kata jirani lakini ndani ya Kata yake wazazi wengi bado hawaoni umuhimu wa elimu hali inayo pelekea baadhi ya wazazi kuwashawishi watoto kujifelisha mitihani ili wabaki nyumbani.
Ameongeza kuwa pamoja na changamoto hiyo wameendelea kuwaelimisha umuhimu wa elimu na kuhakikisha Kila mtoto anaenda shuleni.
Nao baadhi ya wazazi katika Kata ya Kombolinga wamesema baadhi ya sababu zinazo pelekea watoto wengi kutoendelea na masomo ni mwamko mdogo wa wazazi juu ya elimu pamoja na ugumu wa maisha .
Taswira ya habari imefanikiwa kumnasa Kijana mmoja ambaye hakuendelea na masomo ya sekondari na kudai kuwa chanzo kikubwa ilikuwa na Hali ngumu ya maisha ya nyumbani .