Mabadiliko ya tabianchi yanaathirije upatikanaji wa chakula?
20 July 2026, 18:00

Wanasayansi wanabashiri kwamba ongezeko la joto na mabadiliko ya mienendo ya mvua huenda yakaathiri uzalishaji hasa katika maeneo yenye matatizo.
Na Mariam Matundu.
Uhakika wa upatikanaji chakula huathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi kwani ukame, mabadiliko ya vizio vya joto, moto wa nyikani, matukio ya hali mbaya ya hewa, wadudu waharibifu wa mazao, magonjwa na mafuriko yanaweza kuharibu mazao ya chakula.
Uhakika wa upatikanaji chakula huathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi kwani ukame, mabadiliko ya vizio vya joto, mioto ya nyikani, matukio ya hali mbaya ya hewa, wadudu waharibifu wa mazao, magonjwa na mafuriko yanaweza kuharibu mazao ya chakula.
Jambo hili linaongeza matatizo katika mgogoro ambao tayari upo ulimwenguni wa chakula, kwani chakula kikuu kama vile mpunga, ngano na mahindi vinaathirika.
Kuongezeka kwa tatizo la utapiamlo kunaweka afya na maisha ya wanawake na watoto katika hatari na kuongeza mzigo kwa watu wanaoishi na VVU wanaotumia dawa za kupunguza makali ya virusi, kwani mlo kamili kwao ni muhimu ili tiba yao ifanikiwe.