Kaya maskini Dodoma kunufaika na TASAF
18 August 2026, 16:40

Utekelezaji wa mpango watatu unatarajiwa kugharimu dola za kimarekani Zaidi ya milioni 650 ambapo utanufaisha Zaidi ya kaya milioni 1.5 zenye uhitaji Tanzania bara na Zanzibar.
Na Anwary Shaban.
Kaya maskini jijini Dodoma zinatarajia kunufaika na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF kwa kipindi cha miaka minne na kuondokana na utegemezi.
Mpango huo unatekelezwa kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2026 hadi 2030 ukilenga kubadilisha maisha ya kaya maskini kwa kuzipatia fursa zitakazo wawezesha kuongeza kipato na kujenga uwezo wa kujitegemea badala ya kuwa kwenye mpango kwa muda usio na ukomo.
Nao baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wameishauri TASAF kuimarisha mifumo ya ufatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mpango huo ili kuhakikisha kaya zinazonufaika zinafikia malengo yaliyo wekwa na hatimaye kuondokana na umaskini kwa malengo endelevu.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw.Machano Said amepongeza TASAF kwa mchango wake katika kupunguza umaskini katika kaya maskini nchini, kwani utekelezaji wa program hiyo umeendelea kutoa fursa kwa wananchi
Baadhi ya wananchi wanasema TASAF imekuwa msaada kwao hasa kwa kaya maskini kwani imesaidia kaya hizo kujitegemea kiuchumi.