Dodoma FM

Jamii na viongozi Dodoma watakiwa kuhakikisha watoto wanapata chanjo

21 August 2026, 18:16

Picha ni wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ya Mkoa (PHC),.Picha na Elizabeth Tanzania.

Ili kuhakikisha hakuna mtoto anaye achwa nyuma, mkoa umeandaa mikakati ya ziada ya kijiografia ikiwemo kutuma timu maalumu kwenye maeneo ya pembezoni na yaliyo magumu kufikika kama vile kata ya Mangaliza kule Mpwapwa.

Na Elizabeth Tanzania.

Wazazi,walezi, na viongozi mbalimbali mkoani Dodoma wametakiwa kuhakikisha kuwa watoto wote walio zaliwa kuanzia mwaka 2016 wanapata chanjo ya polio ya matone.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ya Mkoa (PHC), Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma ameeleza kuwa, ingawa ni takribani miaka 30 tangu nchi ilipo mpata mgonjwa wa mwisho wa polio mnamo Julai 1996, serikali haitasita kuendeleza afua hizi za kinga.

Dkt. Kazungu amesisitiza kuwa chanjo hiyo ya matone ni salama, haina malipo, na itatolewa kwa ufanisi mkubwa ili kuzuia virusi hivyo visisambae kutoka kwenye mazingira kwenda kwa binadamu.

Kampeni hii kubwa inayo husisha mikoa 8 ikwemo mkoa wa Dodoma imepangwa kutekelezwa kwa awamu mbili tofauti ili kuhakikisha watoto wote wanapata kinga thabiti, ambapo awamu ya kwanza itaanza tarehe 27 hadi 30 Agosti, na awamu ya pili itafuata tarehe 29 Septemba hadi tarehe 2 Oktoba mwaka huu wa 2026.

Kwa upande wa kitaalamu, Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Dodoma, Francis Bujiku, amebainisha kuwa kampeni hii inatumia chanjo maalumu ya matone inayo lenga kumkinga mtoto dhidi ya kirusi cha polio aina yapili.

Bujiku amesema kuwa mkoa umepokea jumla ya dozi 1,076,000 za chanjo na kusamba za timu 2,001 za uchanjaji katika halmashauri zote nane, ambapo kila timu inajumuisha mtoa huduma wa chanjo, mtunza kumbukumbu au takwimu, na mhamasishaji.

Sauti ya Dkt Bujiku.