Matumizi ya simu na kompyuta bila kikomo yatajwa kuharibu afya ya macho
11 September 2026, 16:27

Wazazi na walezi wanahimizwa kuwaongoza watoto katika matumizi yenye mipaka ya simu, kompyuta na televisheni, huku watoto na vijana wakitakiwa kupumzisha macho mara kwa mara na kutumia muda wao pia katika kujifunza, kucheza na kufanya shughuli nyingine nje ya skrini.
Na Elizabeth Mwinuka.
Imeelezwa kuwa matumizi ya vifaa vya kielekroniki kama simu, televisheni na kompyuta kwa muda mrefu bila kuweka mipaka vinaweza kupelekea macho kuchoka .
Baadhi ya wazazi na vijana wanaeleza kuwa matumizi ya muda mrefu ya simu, televisheni na kompyuta yamekuwa yakiongezeka, huku baadhi yao wakiona mabadiliko kama uchovu wa macho na kukaa muda mrefu kwenye skrini.
Mtaalamu wa afya ya macho kutoka hospitali ya Kitete Dkt. Erick Mhando anaeleza kuwa mwanga wa skrini na kuangalia kifaa kwa muda mrefu kunaweza kufanya macho kuchoka, hasa pale mtu anapokaa muda mrefu bila kupumzisha macho yake.