Wazazi Idifu wakwamisha watoto kujiunga kidato cha kwanza
14 September 2026, 16:24

Atanasio Mnyepembe Mwenyekiti kutoka Kijiji cha Idifu ni shuhuda wa mwenendo wa elimu katika kijiji chake, anakiri kuwa licha ya kutumia nguvu nyingi kuhamasisha wananchi kupeleka watoto mashuleni lakini bado kuna mapungufu hasa kwa watoto wanaojiunga na kidato cha kwanza.
Na Victor Chigwada.
Baadhi ya wazazi wametajwa kukwamisha watoto wanaohitimu elimu ya msingi kushindwa kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na taama ya kuwatumia watoto hao kujipatia kipato.
Taswira ya habari imezungumza na wadau wa elimu ambapo wanasema baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kuwaficha watoto wanapo chaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari na kuwatumia kwenye maslahi yao binafsi,
Wamesema ni wajibu wa kila mzazi na jamii kuhakikisha kila mtoto anae takiwa kusoma anakuwa shuleni.