Dodoma FM

Vijana waonywa kuporomoka kwa Maadili

3 May 2023, 4:39 pm

Uvaaji wa nguo zisizo na maadili kwa vijana pia unatajwa kuchochea mmomonyoko wa maadili .

Wamewashauri wazazi kukagua matumizi ya vipindi vya Televisheni majumbani mwao ili kuwaepusha watoto na vipindi viovu vinavyoweza kuharibu maadili yao.

Na Bernad Magawa.

Katika kuhakikisha kuwa Taifa linaendelea kuwa na vijana wenye maadili, baadhi ya wazee Wilayani Bahi wameiomba serikali kuona namna ya kutunga sheria ya mavazi.

Wakizungumza na kituo hiki wilayani Bahi wazee hao wamewataka vijana kujiepusha na mambo yanayodhalilisha utu wao yakiwemo uvaaji wa nguo nusu uchi na kuharibu miili yao kwa kujichora alama mbalimbali na kuacha kabisa kurusha picha za utupu kwenye mitandao ya kijamii kwani siyo maadili ya kitanzania.

Sauti za wazee.

Aidha wameeleza kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya vijana kuiga tamaduni zinazo kinzana na mila za kiafrika kwani ni hatari kubwa kwa vizazi vijavyo huku wakisisitiza wazazi kutimiza wajibu wao kikamilifu katika malezi.

Sauti za wazee