Dodoma FM

Yafahamu madhara yatokanayo na saratani ya mlango wa kizazi

7 February 2024, 5:54 pm

Picha ni Neema Msemo kutoka kituo cha Afya Makole akieleza madhara ya Saratani.Picha na Yussuph Hassan.

Na Yussuph Hassan.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, saratani inayoongoza nchini ni ya mlango wa kizazi kwa asilimia 25, matiti asilimia 10, tezi dume asilimia 9, mfumo wa chakula asilimia 6.5 na saratani nyinginezo.

Wanawake wenye umri kuanzia miaka 23 hadi 45 wametajwa kuwa katika kundi la watu walio katika hatari ya kupata ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi huku ikiambatana na madhara mbalimbali.

Neema Msemo kutoka kituo cha afya Makole leo anaeleza madhara anayoweza kuyapata mtu aliyechelewa kupata matibabu ya Saratani ya Mlango wa Kizazi.

Ameongeza kuwa bado kuna uelewa mdogo kwa jamii juu ya Saratani ya mlango wa kizazi na kusababisha watu kuchelewa kupata matibabu.