Dodoma FM

Wakazi wa Babayu waiomba serikali kuwapelekea huduma ya maji safi na salama

2 November 2021, 11:16 am

Na;Mariam matundu .

Wakazi wa kijiji cha Babayu wilayani Chemba wameiomba serikali kuwaletea huduma ya maji safi ili kupunguza adha wanayokutana nayo katika kutafuta maji umbali mrefu.

Baadhi ya wakazi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema wamekuwa wakitumia zaidi ya saa 3 kufuata maji ambapo pia si maji safi ambayo anawasababishia magonjwa ya matumbo .

Aidha wamesema kutokana na wao kutumia muda mrefu kutafuta maji wamekuwa wakishindwa kutimiza majukumu mengine ya kifamilia na hata kusababisha migogoro .

Kwa upande wake diwani wa kata ya babayu amesema tayari amewasilisha kwa mamlaka ya maji Ruwasa na kwamba wanasubiri bajeti ili usambazaji wa maji uanze mara moja .

Amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati suala hilo likishughulikiwa na kuwasisitiza kuchemsha maji ili kuepuka magonjwa mbalimbali.