Dodoma FM

Wizara ya kilimo yafanya tathmini utoshelevu wa chakula nchini

27 November 2023, 12:42 pm

Picha ni viongozi na wadau mbalimbali walioshiriki katika Mafunzo yaliyoandaliwa na AMDT, Novemba 22,2023 jijini Dodoma.Picha na Alfred Bulahya.

Amesema moja ya changamoto inayokwamisha upatikanaji wa masoko ya uhakika nje ya nchi ni kukosekana kwa tija hii inasababishwa na kutokidhi viwango vinavyotakiwa kuanzia kweye ubora,wingi,mabadiliko ya bei sokoni na kuhakikisha kuwa muda wote tunasambaza bidhaa masokoni.

Na Alfred Bulahya.

Wizara ya Kilimo imefanya tathmini ya hali ya utoshelevu wa chakula nchini katika  kipindi cha mwaka  2003 mpaka  2024 ambapo 2003/2004 utoshelevu wa chakula ilikuwa ni asilimia 96 na Mwaka 2023/2024 ni asilimia 124 huku lengo ni kufikia asilimia 130 kutokana na ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza katika Mkutano wa Mafunzo kwa wadau wa kilimo yaliyoandaliwa na AMDT, Novemba 22,2023 jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Mkurugenzi wa Idara ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo Bw.Nyasebwa Chimagu amesema kuwa Muelekeo wa kilimo nchini ni KILIMO BIASHARA hivyo chochote kinachozalishwa kiwe ndio chakula, ajira na biashara.

Nyasebwa amesema kwa sasa Wizara ya kilimo inaandaa MASTER PLAN ya maegeuzi ya kilimo nchini  ambayo itakuwa inaitwa  ( TANZANIA AGRICULTURE MASTER PLAN 2050) ambayo itajumuisha malengo yaliyopo katika AGENDA 10/30 na mpango wa pili wa maendeleo  unaondelea

 Amesema kuwa wakati serikali ikielekea kuhitimisha Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2020 – 2025 ndio mwanzo wa maandalizi wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa  mpaka 2050 hivyo nayo Sekta ya Kilimo inaandaa mpango wao ambao utasomana na mpango wa nchi katika sekta zote.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa AMDT Dk.Mary Shetto amesema wanashukuru ushirikiano wanaopata kutoka wizara kilimo katika miradi wanayotekeleza katika maeneo mbalimbali.

Picha ni viongozi na wadau mbalimbali walioshiriki katika Mafunzo yaliyoandaliwa na AMDT, Novemba 22,2023 jijini Dodoma.Picha na Alfred Bulahya.

Awali akizungumza katika Mafunzo hayo kwa wadau wa kilimo, Mratibu wa Mradi wa kujenga kesho Bora (BBT)  Ray Mark amezungumzia utaratiu wa vijana wanaotekeleza mradi huo kupelekwa kwenye mafunzo maalum ya Ukakamavu na Uzalendokweny Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  Ili wasiyatelekeze mashamba watakayopewa bali wyathamini na kuyatunza.

Naye Meneja wa mikopo kutoka benki ya CRDB Kanda ya kati, Sarah Mabula amewataka vijana hao kujiunga kwenye vikundi ili waweze kukopesheka na kuongeza mitaji kwenye uzalishaji wa mazao watakayolima kwa sababu benki hiyo inakopesha wakulima walioko kwenye vikundi peke yake.

 Amesema wakulima wanaokopesheka ni wale ambao mashamba yao yanatambuliwa kisheria kwani wakulima wengi mashamba yao hayajarasimishwa bali wanamiliki kimila hivyo wakijiunga kwenye vikundi inakuwa rahisi kwao kutambulika na kukopesheka.