Dodoma FM

Waziri mkuu aagiza mji wa kiserikali ujengwe kwa kuzingatia upandaji miti

1 June 2022, 3:04 pm

Na;Mindi Joseph.       

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameigiza Wizara ya ofisi ya waziri mkuu ,na katibu wa ofisi ya waziri mkuu ,bunge na uratibu  kwa kushirikiana na timu ya wataalamu wanaosimamia ujenzi wa mji wa kiserikali kuhakikisha wanaujenga mji huo kwa kuzingatia programu za upandaji miti.

Agizo hilo ni miongoni mwa maagizo ambayo yametolewa leo na Waziri Mkuu Majaliwa wakati wa Zoezi maalumu la Upandaji miti katika mji wa serikali mtumba jijini Dodoma.

.

Awali ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jaffo amesema agenda ya mazingira ni kila mmoja huku akimuhakikisha waziri mkuu kuwa wataendelea kushirikiana na wizara zote kwa mambo yote yanayohusiana na mazingira ili kuhakikisha wanakabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

.

Nae Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amesema wakati ujenzi wa miundombinu katika mji kiserikali ukiendelea tayari TFS imekamilisha programu ya uoteshaji wa nyasi yaani Ukoka na Miti .

.

Pamoja na hayo ,Zoezi la upandaji wa miti katika.mji kiserikali (Magufuli city) kufanyika leo ,Vilevile Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekabidhi hati za utunzaji wa miti kwa wizara,na ofisi mbalimbali.