Dodoma FM

Wananchi waendelea kuhimizwa kutumia nishati mbadala

15 May 2023, 7:49 pm

Picha ya nishati mbadala aina ya mkaa unaotengenezwa kwa karatasi . Picha na Alfred Bulahya.

Miongoni mwa madhara hayo ni pamoja na ukame, mafuriko, vimbunga, mioto ya misitu vimeharibu maisha ya mamilioni ya watu na kuwaweka katika hatari zaidi ya kukabiliwa na njaa.

Na Alfred Bulahya.

Wakati mataifa yote ulimwenguni yakipambana kuzuia ongozeko la joto duniani, madhara ya mabadiliko ya tabianchi tayari yanadhihirika wazi katika maeneo mbalimbali ya uso wa dunia.

katika kukabiliana na athari hizo Tanzania ni miongoni mwa nchi za Kiafrika zilizoshiriki Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi katika Jiji la Sharm El Sheikh nchini Misri.

Katika mkutano huo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliongoza ujumbe wa Tanzania na kutoa hotuba yake akielezea hatua za Serikali ya Tanzania katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Katika kulitazama zaidi jambo hilo mwandishi wetu Alfred Bulahya amemtembelea binti anayekabiliana na mabaliliko ya Tabianchi kwa kuhama katika matumizi ya kuni na kuanza kutumia mkaa mbadala unaotengenezwa kwa kutumia karatasi.