Dodoma FM

Upatikanaji wa Maji Mlowa barabarani bado ni changamoto

25 January 2023, 4:40 am

Na; Victor Chigwada.                                             

Licha ya maboresho kufanywa katika kisima cha maji katika kata ya Mlowa barabarani  lakini bado upatikanaji wa huduma ya maji katika kata hiyo unasuasua.

Wananchi wa Kata ya Mlowa barabarani wamesema kuwa licha ya uwepo wa kisima cha maji lakini kimeshindwa kufanya kazi kutokana na kukosa ukarabati kwa muda mrefu

Mwenyekiti wa kijiji  cha Mloda Bw.Adamu Philimini amekiri kukabiliwa na changamoto ya huduma ya maji hali inayodhoofisha kauli mbiu ya Serikali ya kumtua mama ndoo kichwani

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw. Anjero Lukasi amekiri kuwepo kwa changamoto ya maji katika baadhi ya vijiji hali inayosababisha wananchi kununua ndoo moja ya maji kwa bei kubwa

Hata hivyo diwani huyo amesema kuwa mpaka sasa wame fanikiwa kujenga mradi mkubwa wa maji kupitia shirika la kimataifa Innovation of Africa