Dodoma FM

Kero ya barabara Hombolo kutatuliwa baada ya miezi 3

2 May 2024, 5:47 pm

Wakazi wa Hombolo wakiwa katika Mkutano wa kijiji ulio wakutanisha na mkuu wa mkoa .Picha na Yussuph Hassan.

Changamoto ya barabara ya Hombolo imedumu kwa muda mrefu huku wakazi wa eneo hilo wakipaza sauti zao mara kwa mara kuiomba serikali itatue kero hiyo.

Na Mariam Kasawa.
Hatimaye changamoto ya barabara ya kutoka Hombolo kwenda Dodoma mjini yapata ufumbuzi wa kudumu.

Barabara hiyo ambayo ipo katika kiwango cha changarawe imekuwa adha kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo hali inayo pelekea wakati mwingine shida ya usafiri.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemery Senyamule hapo jana alitembelea eneo hilo la Hombolo kukagua miradi mbalimbali katika eneo hilo lakini pia alipata wasaa wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Sauti za wananchi.

Je wataalamu wanazumziaje kero hizi zinazo tolewa na wananchi ikiwemo kero ya barabara ambayo imedumu kwa muda mrefu.

Sauti ya mtaalamu
Wakazi wa Hombolo wakiwa katika Mkutano wa kijiji ulio wakutanisha na mkuu wa mkoa .Picha na Yussuph Hassan.

Naye mkuu wa mkoa wa Dodoma akatoa maagizo kwa wataalam na ahadi kwa wananchi kuwa baada ya miezi mitatu upembuzi ukuhusu barabara utakuwa umekamilika hivyo wawe na subira.

Sauti ya Mh. Rosemery Senyamule.