Dodoma FM

Mlima Mautia umebeba historia ya kipekee ya jiolojia nchini

1 July 2026, 16:43

Picha ni mlima Mautia uliopo Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, ni miongoni mwa maeneo machache duniani yenye urithi wa kipekee wa jiolojia.Picha na Dodoma channel.

Tanzania ina fursa ya kuyatumia kama kivutio cha utalii wa jiolojia na kuongeza mchango wa sekta ya utalii.

Na Anwary Shaban.

Mlima wa Mautia uliopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma umetajwa kuwa moja ya maeneo yenye historia ya kipekee ya kijiolojia nchini, kutokana na kupatikana kwa madini adimu ya yoderaite.

Hali inayoweza kuufanya kuwa kivutio kikubwa cha tafiti za kisayansi na utalii wa jiolojia.

Akizungumza katika mlima huo, Meneja wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania iliyo chini ya Wizara ya Madini, Bw. Maswi Solomoni, amesema moja ya majukumu ya taasisi hiyo ni kufanya tafiti za jiolojia na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu rasilimali za madini nchini.

Aidha, Bw. Solomoni amesema uwepo wa madini hayo unaweza kuifanya Kongwa kuwa kitovu cha tafiti za jiolojia, kwani watafiti kutoka maeneo mbalimbali wanaweza kufika kujionea mabadiliko ya kijiolojia yaliyosababisha madini hayo kupatikana katika eneo hilo.

Pia amesema madini hayo hayajatumika kwa kiwango kikubwa kibiashara au viwandani kutokana na sababu kuu tatu; ni madini adimu, yanapatikana kwa kiwango kidogo sana, na hivyo yana thamani zaidi katika tafiti za kisayansi.

Sauti ya Kina Anwary.