Dodoma FM

Gharama kubwa ya vifaa kikwazo kwa watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa

29 June 2026, 17:52

Serikali imezindua sera ya kusimamia shughuli za walevu ambapo pia inahakikisha kuwa sera hiyo inaweka sawa mapitio ya Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma za watu wenye ulemavu ya 2004.Picha na mtandao.

Hata hivyo, wapo watu wenye ulemavu ambao wameweza kujiajiri na kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi, wakionyesha kuwa kwa kupata mazingira na msaada unaofaa wanaweza kufanikiwa kama wengine.

Na Daniel Njau.

Baadhi ya wananchi wanasema watu wenye ulemavu bado wanakabiliwa na changamoto ya kupata fursa za kujitegemea kutokana na gharama kubwa za vifaa vya kufanyia kazi.

Wananchi hao wanaeleza kuwa bei ya vifaa muhimu vinavyowasaidia kufanya kazi imekuwa kikwazo kikubwa kinachopunguza uwezo wao wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kuongeza kipato.

Akizungumza kuhusu suala hilo, akizungumza mtenda kazi katika chama cha watu wenye ulemavu Bw Felician Mkude. amesema elimu ni moja ya fursa muhimu kwa watu wenye ulemavu, akisisitiza kuwa wana haki sawa na wengine kupata elimu, kufanya kazi, kujiajiri au kuajiriwa bila ubaguzi.

Sauti ya kina.