Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuacha kuwabwagia jukumu la malezi wadada wa kazi

2 June 2026, 17:28

Picha ni Askofu msaidizi wa kanisa katoliki Jimbo kuu la Dodoma  Mhasham Askofu Wilbroad Kibozi.Picha na Steven Noel

Elizabeth na Deogratias  ni waumini  wa kanisa Hilo wamesema wazazi na walezi wa Sasa wanejikita Katika utafutaji na kusahau jukumu la malezi na kuwaachia jukumu hilo wadada wa kazi.

Na Steven Noel.

Askofu msaidizi wa kanisa katoliki Jimbo kuu la Dodoma  Mhasham Askofu Wilbroad Kibozi ameitaka Jamii kujikita Katika malezi yanayoendana na hofu ya Mungu Ili kuwa na taifa lenye tija.

Askofu Kibozi ameyasema  hayo Katika parokia ya Bikra Maria wa Fatima Mpwapwa  alipokuwa akizungumza katika Misa ya Kipaimara.

Amesema ili kuwa na kizazi chenye tija na hofu ya Mungu ni lazima wazazi na walezi kujikita Katika malezi yenye hofu ya Mungu.

Sauti ya kina Noel.