Dodoma FM
Dodoma FM
12 December 2024, 16:55

Wakopaji wengi hawana elimu juu ya matumizi sahihi ya mikopo hiyo.
Na mwandishi wetu.
Baadhi ya wananchi Jijini Dodoma wamesema mikopo umiza maarufu kama kausha damu inalenga kusaidia mahitaji muhimu ingawa wakopaji wengi hawana elimu juu ya matumizi sahihi ya mikopo hiyo.
Wakizungumza na Taswira ya habari, miongoni mwa wananchi hao ni Salma Mgasa na Andrea Fredrick wamesema mikopo hiyo inaumiza baadhi ya familia za wakopaji kutokana na kutokujua lengo la kukopa.