Dodoma FM

Wauguzi na wakunga 4166 kufanya usajili na leseni Decemba 29

27 December 2023, 3:30 pm

Picha ni Kaimu msajili baraza la uuguzi na ukunga Happy Masenga akiongea na waandishi wa habari. Picha na Mariam Matundu.

Baraza la Uuguzi na ukunga Nchini mpaka sasa linajumla ya wauguzi na wakunga 49994 ambao wanatoa huduma kwenye zahanati ,vituo vya afya pamoja na hospitali za wilaya ,mikoa na rufaa.

Na Mariam Matundu.

Wauguzi na wakunga 4166 wanatarijia kufanya mtihani wa uşajili na leseni siku ya ijumaa tarehe 29 /12/2023 .

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kaimu msajili baraza la uuguzi na ukunga Happy Masenga amesema mitihani hiyo itafanyika katika vituo vilivyotambuliwa na kukubalika na baraza katika mikoa saba hapa Nchini.

Sauti ya Bi.Happy Masenga .
Picha ni Kaimu msajili baraza la uuguzi na ukunga Happy Masenga akiongea na waandishi wa habari. Picha na Mariam Matundu.

Aidha amesema mitihani hiyo ni muhimu kwani ndiyo inayowawezesha kupata leseni za kufanya kazi ya Uuguzi na ukunga katika vituo vya afya na hospitali kokote Nchini .

Sauti ya Bi.Happy Masenga .

Amewakumbusha pia wauguzi na wakunga kuzingatia suala la maadili na kwamba baraza limekuwa likiendelea kutoa mafunzo ya kukumbusha suala hilo .

Sauti ya Bi.Happy Masenga .