

7 May 2025, 1:38 pm
Hali ya Uzalishaji wa mazao ya Uvuvi ,Waziri Kijaji amesema umeongezeka kutoka tani ,laki nne na elfu sabini na nne na elfu themanini na moja kwa mwaka 2021 hadi kufikia tani laki tano ,ishirini na mbili na mia saba themanini na nane kwa mwaka 2024.
Na Seleman Kodima.
Katika kuendelea kuimarisha afya ya mifugo hapa nchini,Serikali inatarajia kuandaa mpango wa kuchanja na kuwatambua mifugo yote hapa nchini.
Zoezi hilo linatarajia kuzinduliwa mwezi huu wa Tano hadi Mwezi wa sita ambapo tayari wamezalisha na kusambaza dozi milioni kumi na Tisa na Elfu tisini na Tisa ,Mia mmoja za chanjo ya homa ya mapafu ya Ng’ombe
Akizungumzia mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita mbele ya waandishi wa Habari ,Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dkt Ashantu Kijaji amesema kupitia mazoezi hayo mawili ni moja ya mpango wa serikali kuhakikisha wanafungua zaidi soko la mazao ya mifugo kimataifa kwa kuwatambua na kuwachanja mifugo aina zote hapa nchini.
Dkt Ashantu amesema kupitia zoezi hilo pia wanatarajia kuwatambua na kuwachanja mbuzi na kondoa milioni 17 na elfu ishirini na nne na mia mbili.
Aidha amesema uchanja huo utakuwa na faida kwa taifa ikiwa ni pamoja na kukidhi ma takwa la shirika la afya la wanyama duniani,shirika la biashara dunia ambapo linahitaji Tanzania kuchanja wanyama wake wote kuchanjwa ili kuyafikia vyema masoko ya kimataifa.
Pamoja na jitihada hizo,Serikali imefanikiwa kuimarisha biashara ya Nyama kwenda nje ya nchi ambapo mauzo yameongezeko kutoka tani elfu moja mia saba na sabini na nne kwa mwaka 2020/21 hadi kufika Tani Elfu kumi na tatu mia saba na arobaini na tano nukta tatu,nne kwa mwaka 2023/24.
Kwa upande mwingine ,Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kuimarisha miundombinu ya kuhudumia mifugo kwa kujenga mabwawa 19 ,yenye thamani ya bilioni 10.69 ili kuimarisha upatikanaji wa maji kwa mifugo na kupunguza umbali wa utafutaji wa huduma hiyo kwa wafugaji.
Zaidi ya Hapo Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dkt Ashantu amesema wizara hiyo kwa kushirikiana na taasisi za fedha na wadau wa maendeleo wamefanikiwa kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wafugaji mmoja mmoja ,vikundi vya wafugaji wadogo wadogo ambapo kumekuwa na ongezeko la utoaji wa mikopo hiyo kutoka bilioni 2.19 kwa mwaka 2021 hadi kufika Bilioni 267.09 mwezi march 2025.
Wanufakaji wa mikopo hiyo imefikia Elfu ishirini na mbili mia moja na sitini na tatu ikiwawezesha wafugaji hao kununua ng’ombe wa maziwa,kunenepesha ,ununuzi wa kuku wa mayai na nyama pamoja na uchakataji wa maziwa.
Akizungumzia Sekta ya Uvuvi ,Dkt Kijaji amesema zaidi ya watanzania milioni 6 wanajishughulisha na uvuvi huku ukuaji wa sekta hiyo ni asilimia 1.4 na kuchagia pato la taifa kwa asilimia 1.7