Dodoma FM

Familia yakumbwa na taharuki vitisho vya kuvunjiwa nyumba yao

15 January 2024, 8:56 pm

Picha ni Mwenyekiti wa kijiji cha Vikonje Obeid Majenda akiongea na Dodoma Tv. Picha na Fred Cheti.

Kesi hiyo kwa sasa ipo katika ofisi za ardhi za halmsahauri ya jiji la Dodoma ambapo Dodoma Tv Itaendelea kufatilia sakata hilo ili kujua hatma yake.

Na Fred Cheti.
Familia moja katika kijiji cha Vikonje Wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma imejikuta ikiingiwa na hofu baada ya kupewa kitisho cha kuvunjiwa makazi yao kwa madai ya kuuzwa kwa eneo lao kwa mtu mwengine.

Wakizungumza kwa Masikitiko baadhi ya wanafamilia hao akiwemo Sesilia ulaya pamoja na Leah Ulaya wamedai kuwa eneo hilo ni lao kwani wamezaliwa hapo hivyo wanashangazwa na taarifa za kuuziwa mtu mwingine eneo hilo.

Sauti za wanafamilia hao .
Picha ni eneo hilo ambalo linadaiwa kuuzwa. Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wake Mlalamikiwa anaedaiwa kuuza eneo hilo Kepha John amedai kuwa aliwapa taarifa ndugu wa familia hiyo zaidi ya Mara tatu juu ya umiliki wa eneo hilo kuwa si la kwao lakini hawakumsikiliza ndipo alipochukua maamuzi ya kuliuza eneo hilo.

Sauti ya Kepha John mlalamikiwa.

Nae Mwenyekiti wa kijiji cha Vikonje Obeid Majenda anafafanua zaidi juu ya kile kinachoendelea katika sakata hilo.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Vikonje Obeid Majenda.