Dodoma FM

Masoko ya nje chanzo tikiti maji kuadimika nchini

21 August 2023, 4:04 pm

Wafanyabiashara hao wanasema kwa sasa tunda hilo ni adimu kutokana na wafanyabiashara wanchi jirani kufata bidhaa hiyo hapa nchini. Picha na Kilimo bora.

Tunda la tikiti ni moja kati ya matunda muhimu sana katika afya ya mwanadamu kutokana na madini yaliyo ndani yake kama vile Calcium na vitamin A.

Na Neema Shirima.

Baadhi ya wafanyabiashara wa tunda la tikiti maji katika soko kuu  la majengo jijini Dodoma wameelezea changamoto wanazokutana nazo katika biashara hiyo .

Wakizungumza na taswira ya habari wafanyabiashara hao wamesema kwa sasa upatikanaji wa tikiti maji umekuwa mdogo kutokana na wafanyabiashara wa nchi jirani ikiwemo Kenya kufuata bidhaa hiyo hapa nchini na kuisafirisha kuipeleka nchini kwao hali inayochangia tunda hilo kuadimika sokoni.

Sauti ya Mfanyabiashara.
Kwa sasa watumiaji wa tunda hili wameongezeka baada ya kupata elimu kutoka kwa wataalam wa afya. Picha na Kilimo bora.

Aidha wamesema kwa sasa uelewa wa elimu ya utumiaji wa matunda pia unachangia tunda hilo kuwa adimu kutokana na watumiaji kuwa wengi tofauti na kipindi cha nyuma ambapo watu walikuwa hawajapata elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa matumizi ya matunda katika afya ya binadamu

Sauti za wauzaji wa tikiti

Kwa upande wa watumiaji wamesema kutokana na kuadimika kwa tunda hilo kumepelekea wafanyabiashara kupandisha bei hivyo wanashindwa kumudu kununua tunda hilo kwa sasa.

Sauti za watumiaji wa tikiti