Dodoma FM

Serikali yatenga bilioni 387. 73 kwaajili ya maji vijijini

19 July 2022, 1:35 pm

Na;Mindi Joseph .

Serikali imetenga Shilingi Bilion 387.73 kwa ajili ya uwekezaji wa huduma ya  maji maeneo ya vijijini ili kutatua changamoto inayowakabili wananchi.

Akizungumza leo jijini Dodoma na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali Mkurungezi Mkuu wa Ruwasa Mhandisi Clement Kivegalo amesema katika jitihada za kuwapatia huduma muhimu  wananchi hadi kufikia april mwaka huu hali ya upatikanaji wa maji vijini ilikuwa asilimia 74.

.

Katika hatua nyingine amesema katika mwaka huu wa fedha wanatarajia ongezeko la upatikanaji wa huduma za maji kwa wananchi waishio vijijini kwa asilimia zaidi ya 6.

.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson  Msigwa amesema Ruwasa wanajukumu la kuhakikisha wanamtua mama Ndoo kichwani.

.

Inatarajiwa kuwa Ifikapo mwaka 2025 Ruwasa itafikia zaidi ya asilimia 85 ya utoaji wa huduma ya maji kwa wananch waishio vijijini.