Dodoma FM

Wafanyabiashara Soko kuu Majengo kutembelea hospitali ya Mkoa wa Dodoma

28 April 2023, 4:52 pm

Wafanyabishara wa soko la Majengo Jijini Dodoma wakiwa katika mkutano huo. Picha na Thadei Tesha.

Amesema kutoa mahitaji kwa wagonjwa ni moja ya njia sahihi ya kurudisha fadhila kwa jamii kwa kufanya matendo ya huruma.

Na Thadei Tesha.

Wafanyabiashara katika soko kuu Majengo jijini Dodoma wanatarajia kutembelea na kutoa mchango wa vyakula kwa wagonjwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma General ikiwa ni sehemu ya kurejesha fadhila kwa jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa soko hilo Bw Godson Rugazama amesema zoezi hilo litaenda sambamba na zoezi la uchangiaji damu kwa wagonjwa katika hospitali hiyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa soko la Majengo.

Aidha ameongeza kuwa wanatarajia kuandaa hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya kuchangisha fedha ya kununua gari mbili aina ya costa kwa ajili ya matumizi ya soko ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri mkuu Kassim Majaliwa.

Sauti ya Mwenyekiti wa soko la Majengo