Dodoma FM

Mfahamu mkalimani wa lugha ya alama aliyekuwa na kiu ya kujifunza

26 September 2023, 4:15 pm

Picha ni Bi. Dorcas Minazi mkalimani wa lugha ya alama kutoka jijini Dodoma akizungumza na Dodoma Tv. Picha na Yussuph Hassan.

Dorcas Minaz ni moja kati ya wanawake wanaopambana katika kusaidia jamii ya wahitaji hususani viziwi na amekuwa mkalimani mahiri anayeipenda kazi yake kwa sasa.

Na Yussuph Hassan.

Wakati tukiendelea na simulizi ya Mkalimani Mahiri wa lugha ya alama Dorcas Minaz leo mwandishi wetu Marian Kasawa anaendeleza simulizi hiyo iliyoandaliwa na mwandishi Yussuph Hassan.

Waswahili walinena vyema pale waliposema polepole ndiyo mwendo na mwenye pupa hadiriki kula tamu, safari ya kusaka maisha kwa Dorcas ilisonga licha ya lugha hiyo ya alama kuwa ngeni kwake haikuwa kikwazo kuendelea kujifunza na kupambania ndoto zake.

Dorcas namna alivyokuwa anaendelea kuifahamu lugha ya alama ndivyo ambavyo alibaini kuwepo kwa changamoto za mawasiliano kwa viziwi ndani ya jamii.

Baada ya kuhitimu mafunzo ya ukalimani Dorcas hapa ana wito kwa jamii.