Dodoma FM

Wahanga , ukatili wa kijinsia walalamika kusubirishwa muda mrefu wanapokwenda kupata huduma.

13 May 2021, 1:00 pm

Na;Mindi Joseph.

Moja ya changamoto inayotajwa kuwakabili wahanga wa ukatili wa kijinsia ni kusubirishwa kwa muda mrefu wanapokwenda hospitali kupatiwa matibabu wakati mwingine kutopata matibabu.

Ili kufahamu kiini cha changamoto hiyo na hatua wanazochukua pindi wanapowapokea wahanga wa vitendo hivyo Taswira ya habari imezungumza na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa Dkt.Emmanuel Mbalai.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Wilayani  humo ameeleza kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vimeshamiri licha ya kufanya jitihada mbalimbali kuwasaidia wahanga. 

Debora Marco Nyabahi hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya mwanzo Mjini Mpwapwa  amesema wamekuwa wakihakikisha wahanga wanapata haki zao licha ya changamoto ya mashahidi kutotoa ushirikiano mahakamani na kuchangaia kesi zingine kutofika mwisho na hatimaye kuondolewa.