Dodoma FM

Wananchi waomba serikali iendelee kuwapatia elimu ya katiba

13 September 2023, 1:23 pm

Picha ni mkutano wa vyama vya siasa ambao unaendelea uliofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sept 10. Picha na Maelezo Tv.

Wanasheria wanayo nafasi kubwa ya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya katiba ya nchi ili kuwaongezea uelewa wananchi waweze kutambua haki na wajibu wao.

Na Khadija Ayoub.

Wananchi Jijini Dodoma wameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu juu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwaongezea uelewa juu ya haki na wajibu wao kwa Taifa.

Dodoma Tv imefanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa jijii la Dodoma na nilianza kwa  kuwauliza iwapo wanauelewa wa kutosha juu ya katiba ya Nchini.

Sauti za baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma.

Bi Efrasia Peragus ni Mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu dodoma anasema kuwa wao kama kituo wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuisoma na kuielewa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Sauti ya Bi Efrasia Peragus .
Picha ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiongoe katika mkutano huo wa vyama vya siasa .Picha na Maelezo.

Bi. Efrasia ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kupenda kuisoma katiba ya nchi.

Sauti ya Bi Efrasia Peragus .

Hivi karibuni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia katika ufunguzi wa mkutano maalumu wa baraza la vyama vya siasa nchini alisisitiza wanachi kupatiwa elimu juu ya katiba ya nchi kabla ya kuanza kwa mchakato wa katiba mpya.

Sauti ya Dkt . Samia Suluhu Hassan.