Wazazi wahimizwa kuzungumza na watoto kuhusu elimu ya uzazi
6 August 2026, 17:10

Wazazi na walezi watakiwa kujenga ukaribu na watoto wao ili wawe huru kujadili masuala ya afya ya uzazi, kwasababu mawasiliano ya wazi ndani ya familia ni msingi wa kuwalea watoto wenye uelewa na maadili mema.
Na Daniel Njau.
Wananchi wametakiwa kuwapa watoto elimu ya uzazi wakiwa katika umri unaofaa ili kuwasaidia kuelewa mabadiliko ya kimwili wanayopitia na kujikinga na changamoto zinazoweza kuhatarisha afya na maisha yao.
Baadhi ya wananchi wamesema elimu ya uzazi bado ni mpya kwao, huku wengine wakieleza kutofahamu umri sahihi wa kuanza kuwafundisha watoto kuhusu mabadiliko ya kimwili. Wamebainisha kuwa wazazi wengi bado huogopa kujadili masuala hayo na watoto wao.
Akizungumza mtaalamu wa afya Bi Magreth Mkinga, amesema elimu ya uzazi ni muhimu kutolewa mapema kwa watoto ili kuwajengea uelewa sahihi na kuwasaidia kufanya maamuzi yenye kuwakinga dhidi ya mahusiano ya mapema, mimba za utotoni na ndoa za utotoni.