Maudhui yasiyo faa mtandaoni huathiri saikolojia ya vijana
19 August 2026, 17:04

Katika ulimwengu wa sasa, teknolojia imeleta mapinduzi makubwa, lakini pia imekuja na changamoto kubwa za kiusalama, hasa kwa watoto. Mtandao unawapa watoto fursa ya kugundua mambo mengi, lakini pia unawaweka kwenye hatari ya kukutana na picha za ngono.
Na Grace Budodi.
Vijana wametakiwa kutambua kuwa kutazama maudhui yasiyo faa mtandaoni ikiwemo maudhui ya ngono kunapelekea uraibu na kuathirika kisaikolojia.
Nimewatafuta baadhi ya vijana na kuzungumza nao swali langu kwao lilihoji je wanafahamu madhara yanayo weza kumpata mtu anae tazama maudhui ngono mtandaoni ?
Peter Njau ni Mwanasaikolojia na Mnasihi katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, (Genero ) amesema kutazama maudhui hayo mara kwa mara kunaweza kumfanya mtu kuwa mraibu na kutamani kuiga au kufananisha yale anayoyaona kwenye video hizo na maisha halisi.
Aidha amewashauri watu wanaopitia changamoto hiyo kutokuogopa kutafuta msaada, kwa kuwa kuna njia za kuwasaidia kuondokana na utegemezi huo.