Dodoma FM

Bahi Road walalamika kuziba kwa makaravati ya kupitisha maji ya mvua

6 December 2023, 11:44 am

Picha ni baadhi ya wafanyabiashara wa eneo hilo wakisaidiana kuondoa maji ya mvua yaliyozingira eneo hilo. Picha na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara wa eneo hilo wamelalamika kushindwa kuendelea na biashara zao kutokana na maji kuzingira eneo hilo.

Na Khadija Ibrahim.

Wafanyabiashara katika mtaa wa Bahi road Jijini Dodoma wamelalamikia ujenzi wa kituo cha mafuta katika eneo hilo kilichosababisha kuziba makaravati ya maji na kushindwa kufanya shughuli zao hasa kipindi hiki cha mvua.

Dodoma Tv imefika katika eneo hilo na kushuhudia wananchi hao wakipunguza maji yaliyojaa katika eneo hilo yaliyosababishwa na mvua.

hapa wanaeleza ni kwa namna gani changamoto hiyo inawaathiri

Sauti za wajasiriamali.
Picha ni eneo hilo likiwa limezingirwa na maji . Picha na Thadei Tesha.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wajasiriamali na mafundi katika eneo hilo Bw. Ranford Tumaini naye akawa na haya yakusema

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa huo.