Dodoma FM

Rais Samia Azindua mfumo wa M-mama

6 April 2022, 3:12 pm

Na; Mariam Kasawa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh samia Suluhu Hassani amezindua mpando wa M-mama utao wezesha usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga.

Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Chinangali Park vilivyopo jiji Dodoma ambao umeandaliwa na wizara ya habari, Tamisemi  pamoja na wizara ya Afya huku Rais Samia akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu anaelezea namna sekta ya Afya inavyo fanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuboresha Afya ya mama na mtoto.

Waziri wa habari na mawasiliano Mh. nape Nnauye anaelezea mikakati ya Serikali kuboresha huduma za kielectroniki katika utoaji wa huduma za jamii.

Akizungumzia namna ambavyo ofisi ya Tamisemi imekuwa ikifanya kazi katika kuboresha huduma za afya kwa jamii Naibu Waziri wa Tamisem Mh. Festo Dugange amesema.

Mfumo wa usafirishaji  wa dharula kwa wakina mama wajawazito na watoto wachanga ujulikanao kama M-mama unatarajia kuboresha huduma za Afya kwa mama na mtoto hasa waliopo mbali na vituo vya Afya kwa kurahisisha mawasiano na uchukuzi baina ya muhusika na vituo vya Afya.