Dodoma FM

Wazazi waombwa kuchangia chakula cha Mchana shuleni

4 May 2023, 2:58 pm

Wanafunzi Bahi sekondari. Picha na Bernad Magawa.

Na Bernad Magawa.

Katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wa sekondari wanakuwa makini katika ujifunzaji wawapo shuleni hususa ni nyakati za mchana, wazazi wilayani Bahi wameombwa kuwezesha upatikanaji wa chakula cha mchana shuleni ili wanafunzi waweze kujifunza kwa utullivu.

Akizungumza na kituo hiki alipotembelewa na uongozi wa jumuiya ya wazazi shuleni kwake, Mkuu wa shule ya Sekondari Bahi Frank Mcharo amesema watoto wanapata shida wawapo shuleni kwa kukosa chakula cha mchana na kuwaomba wazazi kuwachangia chakula.

Sauti ya Mkuu wa shule ya Sekondari Bahi.

Katika hatua nyingine wanafunzi wameshauriwa kuwashawishi wazazi wao ili waone umuhimu wa kuchangia chakula kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia kufuatilia vizuri vipindi vya mchana.

Sauti ya Yohana Mgomi mwenyekoti wazazi Wilaya ya Bahi

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, binadamu anapokuwa na njaa kwa kiasi Fulani hupoteza uwezo wa kufikiri hivyo wanafunzi wakipatiwa chakula cha mchana uwezo wao wa kujifunza utaimarika na kufanya vizuri katika masomo.