Dodoma FM

Vitambulisho vya kidijitali ni muhimu kwa wafanyabiashara wadogowadogo

9 February 2024, 6:01 pm

Picha ni baadhi ya wadau wakiwa katika mafunzo ya mfumo wa usajili wa machinga kwa maafisa tehama ,biashara na maendeleo ya jamii katika ngazi za mikoa.Picha na Maendeleo ya Jamii.

Maafisa tehama, biashara na maendeleo ya jamii kutoka mikoa yote nchini wamekutana jijini Dodoma katika mafunzo ya ya mfumo wa usajili wa machinga .

Na Mariam Matundu.
Imeelezwa kuwa vitambulisho vya kidigitali kwa wafanyabiashara wadogowadogo vitawezesha kuwaunganisha wafanyabiashara hao na mifumo mingine ya kimkakati na hivyo itasaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kwao.

Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia ,wanawake na makundi maalum dkt Dorothy gwajima ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya mfumo wa usajili wa machinga kwa maafisa tehama ,biashara na maendeleo ya jamii katika ngazi za mikoa .

Amewataka kwenda kutoa mafunzo kwa maafisa katika ngazi za mamlaka ya serikali za mitaa ili kuwezesha zoezi la usajili kwa wafanyabiashara ndagondogo kwenda vizuri.

Sauti ya Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia ,wanawake na makundi maalum dkt Dorothy gwajima

Aidha amewataka kwenda kutekeleza jukumu hili kwa kuzingatia weledi wa hali ya juu ili kuepusha urasimu katika zoezi la usajili kwa wamachinga.

Sauti ya Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia ,wanawake na makundi maalum dkt Dorothy gwajima

Picha ni Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia ,wanawake na makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima akifungua mafunzo ya mfumo wa usajili wa machinga . Picha na Mariam Matundu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha makundi maalum kutoka wizara ya maendeleo ya jamii Juma Samweli amesema kuwa wameamua kuwatumia maafisa wa serikali ili kubeba dhamana hiyo kwa uadilifu .

Sauti ya Juma Samweli

Baadhi ya Maafisa wanaoshiriki mafunzo hayo wamesema zoezi hilo litakwenda kuchochea maendeo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na kwamba watahakikisha wanatekeleza kwa weledi mkubwa.

Sauti za Baadhi ya Maafisa wanaoshiriki mafunzo hayo