Dodoma FM

Wakandarasi watakiwa kuzingatia matakwa ya jiji la Dodoma

31 October 2023, 10:49 am

Picha ni Mbunge wa jiji la Dodoma ambaye pia ni Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde .Picha na Fred Cheti.

Huu ni mpango wa Uboreshaji wa Miundombinu katika miji ya Tanzania ujulikanao kama TACTIC  unaofanywa na wakandarasi watatu.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amewataka wakandarasi waliopewa miradi ya kujenga miundombinu ya barabara katika jiji la Dodoma kuhakikisha wanazingatia  matakwa ya jiji la Dodoma kuwa na mpangalio wenye  hadhi ya kimataifa.

Mhe Senyamule ameyasema hayo leo jijini Dodoma katika hafla fupi ya kuanza kwa  utekelezaji wa Uboreshaji wa Miundombinu katika miji ya Tanzania ujulikanao kama TACTIC  unaofanywa na wakandarasi watatu ambao ni Mkandarasi mkuu CHINA GEO ENGINEERING co. huku mhandisi Msaidizi akiwa ni kampuni ya HONG KONG IK CONSULTANTS CO.LTD kwa kushirikiana na kampuni ya GAUGE  Pro. LTD.

Sauti ya Mh. Senyamule.

Katika hafla hiyo pia alikuwepo Mbunge wa jiji la Dodoma ambapo ameelezea endapo miradi hiyo itafanyika kwa ufanisi itakuwa na manufaa makubwa katika jiji la Dodoma.

Sauti ya Mh Anthony Mavunde.
Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Semyamule akiongea katika mkutano huo.Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mhe Jabir Shekimweri amewataka wakandarasi hao kutekeleza miradi hiyo kulingana na thamani ya pesa ambayo watapatiwa na si kuleta ujanja katika utekelezaji.

Sauti Mh. Jabir Shekimweri

Akizungumza kwa niaba ya wakandarasi wakuu katika ujenzi wa Miradi hiyo…. amesema kuwa watahakikisha wanaitekeleza kulingana na matakwa ya jiji laDodoma pamoja na kuikamilisha kwa wakati.

Sauti ya Mkandarasi.