Dodoma FM

Mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri shughuli za kilimo-Makala

1 November 2023, 12:37 pm

Mabadiliko ya Tabianchi ni tatizo linaliokabili dunia katika karne ya ishirini na moja na kutokana na athari zake katika nyanja mbalimbali zinazogusa maisha ya binadamu wa kawaida kila siku .Picha na Dira Makini.

Mabadiliko ya Tabianchi ni mabadiliko ya hali ya hewa ya muda mrefu katika eneo fulani (Mkoa, Nchi au Bara) tofauti na iliyozoeleka. Mabadiliko hayo huleta athari katika nyanja za kiuchumi, kimazingira na kijamii.

Na Alfred Bulahya.

Tunapata kusikia kisa cha kijana ambaye ametumia fursa ya kuanzisha kitalu cha miti baada ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kusababisha kushindwa kufanikiwa kwenye kilimo.