Dodoma FM

Vijana jijini Dodoma kufikiwa na elimu ya maambukizi ya vvu

1 December 2022, 8:22 am

Na; Benard Filbert.

Ofisi ya mganga mkuu wa Mkoa wa Dodoma imejipanga kuwafikia vijana ambao wanahisiwa kuwa na virusi vya Ukimwi kwa ajili ya kuwapa elimu katika vituo vya kutolea huduma  rafiki ili kupunguza maambukizi hayo.

Taarifa hiyo imetolewa na Daktari Abdullah Hemed kutoka ofisi ya mganga mkuu mkoa wa Dodoma wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi katika Mkoa wa Dodoma.

Daktari Hemed amesema wanamakadirio ya vijana ambao wanahisiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi katika mkoa katika umri wa miaka 14 hadi 24 ambapo mpaka hivi sasa wamewafikia kwa asilimia 72.

.

Akizungumzia takwimu za maambukizi katika Mkoa wa Dodoma amesema Halmashauri ya Dodoma ina asilimia 3 huku Halmashauri ya Kondoa na Kongwa zikiwa na asilimia 2.

.

Taswira ya habari imezungumza na vijana jijini Dodoma ili kujua ni tahadhari zipi ambazo wanachukua ambapo wamebainisha kuwa.

Ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi Halmashauri ya jiji inachukua tahadhari kadhaa ikiwepo kuhakikisha huduma za upimaji zinapatikana kwa asilimia 98 ikiwepo katika makundi maalumu pamoja na huduma ya JIPIME ambapo kila mtu anaweza kujipima mwenyewe pasipo kufika kituo cha afya.