Dodoma FM

Asilimia 11 ya akina mama nchini hujifungua kabla ya wakati kila mwaka

19 November 2023, 10:53 am

Picha ni Waandishi wa habari na Wakina Mama wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt. Alphonce Chandika,wakati wa  maadhimisho siku ya Kimataifa ya Mtoto Njiti.Picha na Mariam Kasawa.

Siku ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati ilianzishwa kwa nia ya kuelimisha kuhusu kujifungua watoto ambao bado hawajakomaa.

Na Mindi Joseph.

Maadhimisho ya siku ya watoto wanozaliwa kabla ya wakati yalifanyika Nov 17 katika hospital ya benjamini mkapa yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo Vitendo vidogo, matokeo makubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa hospital ya benjamini mkapa Dr. Alphonce Chandika amesema serikali imeamua kuwekeza katika dawa, vifaa tiba na kuwasomesha wahudumu wa afya ili kupata wataalamu na kuokoa maisha ya watoto

Sauti ya Dr. Alphonce Chandika .

Nae mkurugenzi msaidizi idara ya watoto kutoka hospital ya benjamini mkapa Dr. Julieth Lubengula ameeleza sababu zinazosababisha mama kujifungua mtoto kabla ya wakati

Sauti ya Dr. Julieth Lubengula.
Picha ni mmoja wa akinamama ambaye alijifungia mtoto kabla ya wakati(Njiti)akitoa shukrani kwa   Madaktari. Picha na Mariam Kasawa.

Kwa upande wao baadhi ya wakina mama waliojifungua kabla ya wakati (watoto njiti) ambao watoto hao wanaendelea vizuri wanasema watoto hao ni sawa na watoto wengine wanao zaliwa kwa njia ya kawaida

Sauti za baadhi ya wakina mama .

Takwimu zinaonyesha kuwa takribani wakina mama milioni 2 sawa na asilimia 11 wanajifungua kabla ya wakati vilevile takribani watoto elfu hamsini wenye umri chini ya siku 28 hufariki kutokana na changomoto ya kuzaliwa kabla ya wakati

Sauti ya Dr. Alphonce Chandika .
Picha ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya watoto Benjamin Mkapa (BMH),Dkt Julieth Kabengula,akielezea sababu za wanawake kujifungua wataoto kabla ya wakati. Picha na Mariam Kasawa.