

23 April 2025, 6:28 pm
Sanjari na hayo wazazi wamewataka vijana kuzingatia malezi na maadili yanayofundishwa na wazazi wao, na kuongeza kuwa hakuna mzazi anayefurahia kuona mtoto wake anaharibikiwa.
Imeelezwa kuwa katika jamii, vijana wanakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa marafiki, jambo ambalo linaweza kuathiri maamuzi yao katika maisha.
Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya vijana kutoka eneo la majengo jijini Dodoma wamesema kuwa aina ya marafiki inaweza kuwa chachu ya mandeleo au chachu ya kukurudisha nyuma kutokana na ushauri wanaoutoa kwako.
Nao baadhi ya wazazi wamesema ni muhimu kwa vijana kufanya uchaguzi mzuri wa marafiki ili kujifunza mienendo na tabia nzuri kutoka kwao.\par