Dodoma FM

Wakazi jijini Dodoma wameiomba serikali kuangalia upya makato yanayo tozwa kwa sasa katika miamala ya fedha

16 July 2021, 1:43 pm

Na;Yussuph Hans.

Wakazi Jijini Dodoma wamelalamikia ukubwa wa makato yanayotozwa kwa sasa katika miamala ya fedha kwa njia ya simu, huku wakiomba Serikali kuangali tena sheria hiyo upya.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wakazi hao wamesema kuwa makato hayo yanawaumiza kiuchumi hivyo Serikali haina budi kushusha tozo hizo.

Baadhi ya wakala wa huduma za fedha kupitia mitandao ya simu, wamesema kuwa wanahofu na biashara hiyo huenda ikadorora kwa muda, kutokana na malalamiko ya upandaji wa tozo.

Akizungumza na Dodoma Fm mchambuzi wa masuala ya kiuchumi Prof Enock Mwicheche, amesema kuwa sheria imepitia michakato mbambali, hivyo inafaida na hasara zake pia inaweza kuepelekea baadhi ya wafanyabiashara kuathirika na huduma za miamala ya kifedha.

Mfumo mpya wa tozo kwa wale wanaotumia simu za mkononi kufanya miamala ya fedha yaani kutuma na kupokea umeanza kutumika rasmi siku ya jana ni ikiwa ni sheria mpya iliyopitisha katika bunge la bajeti ya 2021/22.