Dodoma FM

Wizara ya Maendeleo ya jamii yaja na kampeni ya SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA MAENDELEO

24 June 2022, 4:15 pm

Na; Bennard Filbert

Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyozinduliwa  na wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto iliyopewa jina la SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA MAENDELEO  TANZANIA inaendelea jijini Dodoma kwa lengo la kutoa elimu katika jamii kukemea vitendo visivyovyakiungwana.

Akizungumza na taswira ya habari Salim Dewiji katibu wa hamasa mkoa wa Dodoma amesema vitendo vya ukatili vimekithiri kwa kiwango kikubwa hali iliyosababisha waziri wa wizara hiyo Doroth Gwajima kuja na kampeni hiyo.

Amesema kampeni hiyo ipo nchi nzima lakini katika halmashauri ya jiji la Dodoma tayari wameanza kutoa elimu.

.

Kadhalika amesema kuwa kampeni hiyo ipo katika ngazi zote za uongozi lengo kuifikia jamii kwa kila namna.

Kadhalika amesema leo hii wanatoa elimu hiyo katika shule ya msingi Ipagala A elimu ambayo itahusisha wazazi na wanafunzi.

.

Malik Masoud ni katibu wa mkoa katika kampeni hiyo amesema wamekuwa wakishirikiana na ofisi ya ustawi ya mkoa ili kushirikiana kwa ukaribu.

.

Kampeni ya SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA MAENDELEO  TANZANIA ilizinduliwa na waziri  wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Dk Doroth Gwajima june 16 katika maadhimisho siku ya mtoto wa afrika.