Dodoma FM

Wakulima wapongeza mfumo wa M-KULIMA

7 August 2023, 2:52 pm

Mratibu wa M-kulima Kanda ya Kati Robert Mbata akiwahamasisha wakulima kutembelea katika banda lao kwenye maonesho ya nanenane kupata elimu kuhusu M-KULIMA. Picha na Mindi Joseph.

M-Kulima ni mfumo unaolenga sekta ya kilimo na unatumika mahali popote kwa mkulima kupokea malipo yake kwa wakati na unarahisisha shughuli za Kilimo.

Na Mindi Joseph.

Wakulima wa zao la Zabibu Mkoani Dodoma wamepongeza uwepo wa mfumo wa M-kulima kwani unamrahisishia Mkulima kupokea malipo yake na kuhakikisha pesa yake inakuwa salama.

Teknolojia hii  imeongeza Tija kwa wakulima kupokea malipo yao kwa wakati kupitia mfumo wa M-kulima.

Wakulima wanasema M-kulima imeondoa changamoto za ukosefu wa taarifa muhimu za Kilimo.

Sauti za Wakulima wa zao la Zabibu.
Picha ni Mkulima akieleza jinsi elimu hiyo itakavyo mnufaisha . Picha na Mindi Joseph.

Mratibu wa M-kulima Kanda ya Kati Robert Mbata amesema lengo la kuwaalika wakulima katika Banda lao Nanenane ni kutoa elimu ya Kutumia Mfumo huo unaomrahisishia mkulima kupokea malipo yake na kuhakikisha pesa yake inakuwa salama.

Sauti ya Mratibu wa M-kulima Kanda ya Kati Robert Mbata .