Dodoma FM

Mlowa Bwawani walalamika ujenzi wa Tanki kutokamilika

26 April 2023, 5:11 pm

Wakazi wa Dodoma Tv wakizungumza na Dodoma Tv. Picha na Alfred Bulahya.

Mradi huo ulitarajiwa kukamilika ndani ya Mwezi mmoja baada ya kutambulisha october 30 2022 lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea kutokana na changamoto mbalimbali.

Na Mindi Joseph.

Wananchi wa Kijiji Cha Mlowa Bwawani Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wamelalamikia kutokukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Tanki la maji ambalo lilitakiwa kujengwa mwezi Oktoba 2022.

Dodoma Tv imezungumza na wananchi hao ambapo hadi sasa bado wamekumbwa na sintofahamu wasijue nini sababu za mradi huo kutokamilika kwa wakati.

Sauti za wananchi

Adrew Mseya ni Diwani wa kata ya Mlowa Bwawani anaeleza jitihada ambazo wamefanya hadi sasa Kuhusu ujenzi huo.

Sauti ya Diwani wa kata ya Mlowa Bwawani.