Dodoma FM

Vijana 300 kunufaika na mradi wa kilimo Bahi

6 July 2023, 4:05 pm

Mradi huo unaofadhiliwa na Baraza la maaskofu la Italia kupitia CMSR Tanzania  ambao utadumu kwa muda wa miaka miwili na  utatekelezwa kwenye kata nane wilayani Bahi. Picha na Bernad Magawa.

Vijana wametakiwa kuimarisha vikundi vyao kwani tayari vimesajiliwa na vinatambulika kisheria.

Na.  Bernad Magawa

Vijana  300 wilayani Bahi watanufaika na mradi wa kilimo kwanza unaowashirikisha vijana kutekeleza shughuli za kilimo kupitia Mashamba Darasa ili kusaidia jamii kuwa na uhakika wa chakula kwa kuzalisha mazao ya bustani pamoja na  zao la mtama linaloendana na hali ya hewa ya mkoa wa Dodoma.

Mradi huo unaofadhiliwa na Baraza la maaskofu la Italia kupitia CMSR Tanzania  ambao utadumu kwa muda wa miaka miwili na  utatekelezwa kwenye kata nane wilayani Bahi ukijumuisha vijana 20 kila kijiji  kutoka vijiji 15 vya wilayani humo.

Akizungumza wakati wa kugawa vifaa mbalimbali vya kilimo kwaajili ya kuwezesha kilimo cha mbogamboga wakati wa msimu huu wa kiangazi vikiwemo mbegu za mbogamboga, madawa ya kuthibiti wadudu, vifaa vya usalam, zana za kilimo, matenki ya kuhifadhia maji pamoja na pampu za kuvuta maji, Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Bahi  Zaina Mlawa amewaasa vijana kutunza vifaa hivyo ili viwanufaishe huku akigawa vyeti vya usajili kwa baadhi ya vikundi.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Bahi.
Baadhi ya vifaa vya kilimo ambavyo vitatumika katika Mradi huo. Picha na Bernad Magawa.

Awali Afisa kilimo, mifugo na uvuvi wilaya ya Bahi Siwajibu alielezea kwa kina namna mradi huo utakavyotekelezwa wa vijana na jinsi utakavyo badili maisha yao huku Muwakilishi wa CMSR Tanzzania Mkoa wa Dodoma akitoa neno naye afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Bahi Denis Komba akasisitiza vijana kuimarisha vikundi vyao kwani tayari vimesajiliwa na vinatambulika kisheria.

Sauti ya Afisa kilimo, Muwakilishi wa CMSR.