Dodoma FM

Wakazi wa Njoge wahofia kuharibika zaidi kwa miundombinu ya barabara msimu wa mvua

19 October 2022, 9:15 am

Na; Victor Chigwada.  

Kuchelewa kwa ukarabati wa barabara za kata ya Njoge umewapa wasiwasi wakazi wa kata hiyo wakati wakijiandaa na msimu majira ya mvua

Wakizungumza  na Taswira ya Habari baadhi ya wananchi wa kata hiyo  wamedai kuwa barabara hizo zimesahaulika hali ambayo inatoa wasiwasi  pindi mvua zinapo kuwa zinanyesha kutokana na ubovu wa barabara hiyo

.

Diwani wa Kata hiyo Bw.Abdala Dedu amekiri kukabiliwa na uchakavu  huo wa miundombinu ambao bado wanajaribu kufuatilia kwa karibu ili kufanya ukarabati kipindi hiki cha kiangazi

Ameongeza kuwa mwingiliano wa mipango kazi ya Serikali ikiwa ni pamoja na sensa huenda  ilikwamisha baadhi ya miradi kuendelea katika maeneo mengi nchini

.

Naye mwenyekiti wa Kijiji Cha Njoge Bw.Peter Mwachahe amesema pamoja na adha hiyo lakini zipo baadhi ya barabara  zinazopitika bila tatizo.

.