Dodoma FM

Watu wenye ulemavu wametakiwa kuchangamkia fursa

24 April 2023, 4:28 pm

Makamu mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya jamii ambae pia ni Mbunge wa viti maalum (CCM) Bi. Riziki Lulida alipo watembelea watu wenye ulemavu. Picha na Fred Cheti.

Kwa Sasa serikali imekuwa ikitoa fursa nyingi ambazo watu wenye ulemavu wanahaki ya kushiriki na kuwataka kuchangamkia kila fursa inayotolewa ikiwemo mikopo ya asilimia 10 ya  halamshauri ambayo kundi hilo litapata asilimia 2 .

Na Fred Cheti.

Wito umetolewa kwa makundi ya watu wenye ulemavu nchini kutumia vizuri fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali kwa kundi hilo ikiwemo mikopo kwa ajili ya kujipatia maendeleo.

Rai hiyo imetolewa na Makamu mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya jamii ambae pia ni Mbunge wa viti maalum (CCM) Bi. Riziki Lulida wakati   Akizungumza na baadhi ya watu wenye ulemavu alipowatembelea na kuwashika mkono kwa baadhi ya mahitaji katika moja ya ofisi zao zilizopo maeneo ya shule ya sekondari viwandani jijini Dodoma.

Sauti ya Bi. Riziki Lulida
Baadhi ya wadau pamoja na watu wenye ulemavu wakiwa katika shule ya sekondari Viwandani. Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wao baadhi ya watu wenye ulemavu katika kituo hicho wameishukuru serikali kwa kuendelea kutengeneza fursa mbalimbali kwa kundi hilo.

Sauti za baadhi ya watu wenye ulemavu .