Dodoma FM

Wananchi Bahi watakiwa kutunza chakula

12 July 2023, 1:41 pm

Afisa kilimo kata ya Bahi bi. Mariam Joshua akizungumza na wakazi wa Nagulo Bahi. Picha na Mariam Kasawa.

Mara nyingi jamii imekuwa ikishauriwa kuhifadhi sehemu ya mavuno ya mazao ili kusaidia upatikanaji wa chakula cha kutosha katika familia na kuepusha hali ya kuanza kuwa tegemezi kutokana na kuuzwa kwa mazao yote.

Na Mindi Joseph.

Wakulima Kata zote Wilayani Bahi wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kuuza chakula pamoja na kutumia chakula kingi kwa ajili ya shughuli za jando kwa watoto wao.

Ni Msimu wa mavuno katika maeneo mbalimbali lakini hali ni tofauti kwa wakazi wa Nagulo Bahi baada ya kuvuna mpunga kwa wingi sherehe za jando zimekuwa nyingi huku baadhi wakiuza mazao kwa fujo na kutumia pesa kushinda minadani na katika vilabu vya pombe.

Bi. Mariam Joshua ni Afisa Kilimo Kata ya Bahi amesema wakulima wanapaswa kutambua thamani ya kutunza chakula ili kiwe msaada kwao hapo badae.

Sauti ya Afisa kilimo.
Baadhi ya wanaume wa kijiji hicho cha Nagulo wakiwa katika mkutano wa kijiji. Picha na Mariam Kasawa.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa kata ya Bahi Agostino Ndonuu amewataka wananchi kutotumia chakula kingi kwa ajili ya shughuli za jando kwa watoto na wale wenye tabia ya kuuza mazao na kuzunguka minadani kunywa pombe waache tabia hiyo.

Sauti ya diwani kata ya Bahi.