Dodoma FM

Tabia bwete yatajwa chanzo cha ugonjwa wa kisukari

15 February 2024, 5:01 pm

Baadhi ya wananchi wamezungumzia uelewa wao kuhusu Ugonjwa wa Kisukari.Picha na Mindi Joseph.

Ili kuepuka magonjwa yanayosababishwa na mtindo mbovu wa maisha ni muhimu kufanya mazoezi ya wastani ya dakika 35 hadi 45 mara kwa mara.

Na Mindi Joseph.

Imeelezwa kuwa tabia Bwete ikiwemo kutofanya mazoezi unene uliopitiliza,kula vyakula vya wanga na mafuta kwa wingi  ni chanzo cha ugonjwa wa Kisukari.

Ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoua kimya kimya katika kundi hili la magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Watu milioni 285 Duniani kote wameathiriwa na kisukari ambayo ni sawa na asilimia 6.6 ya idadi ya watu wote ulimwenguni.

Picha ni Alemiana Alex  ni Daktari kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma. Picha na Mindi Joseph.

Kuepuka uvutaji wa singara na unywaji wa pombe kupita hatari inasaidia kukabiliana na ugonjwa huo

Alemiana Alex  ni Daktari kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma  anashauri nini kifanyike.

Sauti ya Alemiana Alex  ni Daktari kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma .

Nao baadhi ya wananchi wamezungumzia uelewa wao kuhusu Ugonjwa wa Kisukari.

Sauti za wananchi.