Uhaba wa walimu wapelekea wazazi Mguba kuchanga 1000 kila mwezi
30 July 2026, 17:36

Jitihada za kumpata mwalimu mkuu wa shule hiyo kueleza changamoto hiyo ya walimu na malalamiko ya wazazi haikuweza kufanikiwa.
Na Victor Chigwada.
Uhaba wa walimu katika shule ya msingi Majengo iliyopo kijiji cha Mguba wilayani Chamwino umepelekea kila mzazi kuchangia shilingi 1000 kila mwezi kwaajili ya kuwalipa walimu wanao jitolea shuleni hapo.
Hali hiyo imekuwa ikiwapa wakati mgumi wazazi wenye mtoto zaidi ya mmoja shuleni hapo kwa hhujikuta wakitumia gharama kubwa kila mwezi kwaajili ya mahitaji ya wanafunzi na kulipa mchanho huo wa kuwalipa walimu.
Wakiongea na taswira ya habari baadhi ya wazazi wameiomba serikali kutafuta suluhu ya changamoto hiyo ikiwemo kuajiri walimu wa kutosha shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mguba bw. Amekiri shule hiyo kukabiliwa na upungufu wa walimu hali inayo walazimu kuchangisha fedha ya kuwalipa walimu wa kujitolea kila mwezi ambapo kila mzazi mwenye mtoto shuleni hapo hulazimika kutoa shilingi elfu moja.
Aidha ameongeza kuwa michango hiyo ya shilingi elfu Moja imekuwa changamoto Kwa wazazi na kupelekea kuibua malalamiko juu ya suala hilo